Katika ujenzi kila kazi/kitu kina muda wake mfano huwezi peleka mabati kwenye eneo unalojenga(site) wakati ndiyo kwanza unachimba msingi hivyo basi hata mfumo wa umeme unamuda wake.
Kumbuka: Lengo la kukuwekea mada hii ni kukupa a,b,c.. wewe unayefikiria kujenga au umeshajenga sasa unataka kufanya marekebisho(maintenance).
Wakati wa kuanza
kuweka mfumo wa umeme kwenye nyumba.
Baada ya mchoro wa umeme
kukamilika (electrical drawing) unaoonesha jinsi mfumo wa umeme utakavyopita
kwenye nyumba yako, mfumo huu unaanza kuwekwa katika ngazi zifuatazo;
Mfano wa mchoro wa umeme
-
Kabla ya kupiga lipu(plaster) – Huu ndiyo wakati wa awali kabisa wa kuanza kuweka mfumo wa umeme ambapo mafundi umeme hupitisha mabomba na vibox vya kuwekea switch,socket na distribution box (db).
Jinsi mabomba ya umeme yanavyopitishwa
-
baada ya kufanya umaliziaji(finishing) ya ukuta na kuweka ceiling/gypsum board – wakati huu ndiyo wa mwisho kumalizia kuweka(install) mfumo wa umeme ambapo mafundi umeme wanapitisha nyaya na kupachika taa, switch, socket, nk .
switch
Kumbuka:
kama utaratibu huu hautafuatwa basi itabidi mafundi umeme watindue ili
kupitisha mabomba wakati umeshafanya umaliziaji (finishing).