Showing posts with label apps&soft. Show all posts
Showing posts with label apps&soft. Show all posts

Saturday, 28 September 2019

Apps bora kwa watumiaji wa simu za Iphone

Hivi unajua ni kazi ngumu sana kupekua katika Appstore na kuanza kushusha Apps nyingi nyingi ili upate moja ile ambayo ni nzuri?


Mbali na hapo kama hujawahi kuisikia App ikisifiwa na baadhi ya watu ndio itakua vigumu kabisa kuweza kuelewa kama App hiyo itakua ni nzuri ama la!
Lakini hata hivyo tafiti zimefanyika kwa wale watumiaji wa simu za iOs ni swala ni kwamba, App bora za mwaka 2016 zimefahamika
Fanya Uchunguzi Wa Kina Wa App Kabla Ya Kuishusha
Fanya Uchunguzi Wa Kina Wa App Kabla Ya Kuishusha
Mwingine anaweza akajiuliza ubora wa App uko wapi? Kwa leo sina majibu ya moja kwa moja lakini ningependa tuzione App hizo labda utajifunza kitu
• Evernote
Evernote
Evernote
Hii ni App moja maarufu sana ambayo inamuwezesha mtuamiaji kuweza kuitumia katika kuandika ‘note’ katika kifaa chake. Yaani mtu utakuwa huna haja ya kutembea na peni na daftari au kitu chochote cha kuandika.

Vilevile uzuri wa Evernote ni kwamba hata siku moja huwezi ukapoteza kile unachokiandika miaka na mika kwa sababu unaweza ukakihifadhi katika ile hifadhi ya mtandao (Cloud) na jambo hili ni tofauti kabisa na njia za kawaida tunazotumiaga. Fikiria labda umeandika kitu chako katika daftari lako la kumbukumbu alafu ukalipoteza daftari hilo au labda panya wenye njaa kali wakapita nalo!
• Waze
Waze
Waze
Kwa wale wote ambao wanapenda kusafiri hii sio App ya kuikosa kabisa, hata kwa wale watu ambao kidogo hawaijui mitaa vizuri hii ni App moja ambayo ni nzuri sana kwa ajili yao. Kwa kutumia App hii hata waendesha magari na vyombo vingine vya moto wanaweza wakatonyana mahali ambapo kuna askari wa barabarani. App hii ya Waze ina uwezo wa kujua dereva anaendasha kwa spidi ya kiasi gani na kutoa ushauri kadha wa kadha kuhusiana na barabara.
• 1Password
1Password
1Password
Je wewe ni mmoja kati ya wale ambao kila siku wanasahau password zao? Nawajua watu wengi sana wanaosumbuliwa na hii kitu. Kuna siku simu yangu iliishiwa na chaja nikaomba kwa rafiki yangu iki niingine katika matandao mmoja wa kijamii, ila alichinijibu ni kwamba siwezi fanya hivyo kwani yeye haikumbuki Password yake.
Kwa kutumia 1Password zoezi zima litarahisishwa kwani mtu utakua na kazi ya kuikumbuka password moja tuu na kisha 1Password ndio itachukua jukumu zima la kuzikumbuka password zinigne zote
• IFTTT
If This, Then That (IFTT)
If This, Then That (IFTT)
Wengi wanapata shida na wengine hawajui kabisa ‘if this, then that’ ni kitu gani. Kwa upande wangu sijawahi kutumia App ambayo imetengenezwa kwa akili kama hii. Lakini kumbuka pia tuna mitazamo tofauti tofauti. App hii ukiwa nayo unaweza ukaamuru vitu vingi kufanyika, kwa mfano unaweza ukaamua kuwa kila ukituma picha yako katika mtandao wa kijamii wa Instagram basi picha hiyo ijihifadhi katika hifadhi ya mtandao kama vile Google Drive. Kuna machaguzi mengi unaweza kufanya ukiwa unatumia App hii utaweza kufanya jambo moja na kufanya lingine litokee.
• SwiftKey
SwiftKey
SwiftKey
Hii ni ‘keyboad’ mbadala na kama ukiniuliza mimi basi hii ndio bora kuliko zile zingine zote. Kumbuka kwa kipindi cha muda mrefu sana Apple ilikua hairuhusu utumiaji wa ‘keyboard’ zingine isipokuwa zile ambazo wanatengeneza wao tuu. Hii ilikuja ikabadilika na ndipo hapo Swiftkey walipoingia. Mpaka sasa ndio ‘keyboard’ bora ya mbadala kwa simu za iPhone
• WhatsApp


Hapa sina hata haja ya kuuelezea mtandao huu sana, kwani naamini kila mmoja wetu angalau anautumia mtandao huu kuwasilina na ndugu, jamaa na marafiki. Pia vile vile mtandao huu unajijua kama uko juu ndio maana kila siku unaongeza vipengele mbali mbali ili kuhakikisha kuwa bado unabaki kuwa juu. Hivi karibuni kipengele cha kupiga simu za kuonana kimeongezwa katika mtandoa huo
• Prisma
Prisma
Prisma
Prisma ni moja kati ya App ambazo zimejipatia umaarufu wake katika kipindi cha muda mdogo sana kulinganisha na Apps zingine nyingi ambazo zilisota sana kabla ya kujulikana. Prisma ni App ya kuhariri picha na kuzifanya kuwa na muonekano wa kipekee kabisa
• Snapchat
SnapChat
SnapChat
Snapchat ni mtandao wa kijamii kama vile Instagram tuu lakini mtandao huu uliingia sokoni na kuleta changamoto nyingi sana kwa wapinzani wake kama vile Facebook. Mtandao huu ulipoanza kuliteka soko kwa kiasi flani ndipo hapo mitandao mingine ilipoamua kubadilika na kuongeza vipengele vingine ambavyo pia vilikua vinapatikana katika mtandao huo au la!
• App Za Nyongeza
App ziko nyingi sana ambazo ni nzuri na zimefanya vizuri mwaka 2016 katika simu janja za iPhone, App kama Facebook, Spotify, Adobe Photoshop Fix n.k
Hivi umefikiria kichwani App ambayo unaona imefanya vizuri katika simu za iPhone na haijatajwa hapo juu, kuwa na amani kuitaja hapo chini sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako

komputer yako inasumbuliwa na virus CCleaner ndo mkombozi soma zaidi.......

CCleaner ni moja ya programu maarufu kwa ajili ya kuwasaidia watumiaji wa kompyuta – kwa Windows na Mac, kusafisha kompyuta zao kwa kuondoa mafaili ya uchafu na yanayojaza nafasi kwenye kompyuta. Ila imefahamika hivi karibuni CCleaner ndiyo ilikuwa ni kirusi pia.

Watafiti wamegundua wadukuzi walifanikiwa kuingia kwenye mtandao wa kampuni inayotengeneza programu hiyo maarufu na kisha kubadilisha faili la programu hiyo kwa kuweka faili ambalo ndani yake wameweka kirusi kwa ajili ya kuathiri kumpyuta za watakaodownload na kutumia programu hiyo.

CClearner ni progrmu (haiuzwi) maalum kwa ajili ya kuondoa cookies kwenye kompyuta na toleo lake la v5.33.6162 lilikuwa na dosari baada ya programu hiyo kudukuliwa na kirusi kuwekwa ndani yake. Takribani wateja mil. 2.2 waliokuwa wamepakuwa toleo la CCleaner v5.33.6162 waliathiriwa na kirusi hicho.
Kompyuta zilizokuwa zimewekwa programu ya CCleaner yenye kirusi ilikuwa ikichukua taarifa za kompyuta husika zilizojumuisha: jina la kompyuta, utambulisho wa kompyuta husika kwenye mtandao (IP address), programu ziliwekwa kwenye kompyua husika, n.k na kuzipeleka taarifa hizo kwenye server iliyopo Marekani.
CCLeaner
CCLeaner ni programu inayomilikiwa na Avast na ni moja ya programu iliyopakuliwa na watu wengi zaidi. Ipo katika orodha ya programu za kuaminika.
Kirusi hicho kwenye CCleaner tayari kimeshaondolewa kabla ya kuweza kuleta madhara makubwa kwa watumiaji wa programu hiyo. Imekuwa tabia ya wadukuzi wengi kuanzia mwaka 2016 kudukua programu zenye watumiaji wengi (CCleaner imepakuliwa zaidi ya mara bil. 2).

Ni vyema ukaingia gharama ukanunua vitu ambavyo vina dhamana kuliko kupakua programu ya bure kutoka kwenye mtandao; mara nyingi programu hizo huwa ni rahisi kudukuliwa na kuweza kusababisha madhara kwenye kifaa chako.

huawei mate 20x simu janja sokoni

Dunia nzima inafahamu vuta nikuvute/vikwazo ambavyo Huawei Technologies imekuwa ikikumbana navyo kwa miezi kadhaa kitu ambacho kimechelewesha kuingia sokoni kwa bidhaa mbalimbali hasa zinazotumia 5G.

Tulishaandika mara kadha kuhusu Huawei na simu janja zenye teknolojia ya 5G ingawa zilikuwa bado hazijaingia sokoni mpaka kumi la pili kwa mwezi Julai; Huawei Mate 20X yenye 5G ilitakiwa kuzinduliwa mwezi Juni huko Uingereza lakini kutokana na sababu mbalimbali hilo halikuwezekana. Hata hivyo, inaonekana mambo yameanza kuinyookea kampuni husika kwani simu hiyo imeingia sokoni UK na Umoja wa falme za Kiarabu (UAE).


Je, sifa zake ni zipi?

Huawei Mate 20X (5G) ni simu ambayo bado uzinduzi wake haujafanyika ingawa tayari sifa muhimu zimeshafahamika:
Kipuri mamaBalong 5000 (ndio inayowezesha teknolojia ya 5G kwenye simu husika)
Urefu wa kioo: inchi 7.2 (OLED)
Memori: RAM-GB 8, diski uhifadhi-GB 256
Kamera: Nyuma zipo 3-MP 40, MP 20 na MP 8. Mbele ipo moja-MP 24

Betri: 4200mAh na teknolojia ya kuchaji haraka kiwango cha 40W
Mtandao+Programu endeshi: GSM / HSPA / LTE / 5G. Itakuwa inatumia Android 9
Huawei Mate 20X
Huawei Mate 20X (5G) ambayo pia inatumia kalamu janja.

Mpaka sasa rununu (simu janja) husika imeingia sokoni kwenye nchi za Falme za Kiarabu kwa $960|Tsh. 2,246,400. Kiujumla simu husika itazinduliwa Julai 22 2019, Julai 26 itazinduliwa nchini Uchina na itauzwa $1,240|Tsh. 2,901,600.

Sunday, 22 October 2017

Matumizi ya Kadi za Benki katika Manunuzi Kwenye Mtandao

matumizi-ya-kadi-za-benki
Teknolojia inayowezesha matumizi ya kadi za benki kununua bidhaa katika maduka na mtandao wa kompyuta ni kitu kilichozoeleka na kufanyika sana katika nchi zilizoendelea hasa Ulaya na Marekani.
Lakini kwa Afrika ikiwemo Tanzania si jambo la kawaida sana. Japo kuna watu wachace ambao wanatumia.
Kuna fursa nyingi katika utumiaji wa kadi za benki kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma,ikiwemo kununua bidhaa toka nje kwa bei nafuu ukilinganisha na kununua kwa wachuuzi wa maduka.
Bidhaa hasa za kielektroniki kama vitabu na programu za kompyuta au simu zinapatikana kwa urahisi kutoka katika masoko kupitia mtandao wa kompyuta.
Biadhaa nyingine ni zile halisi kama kamera,simu,komputa,vitabu na vingine vingi kutaja vichache vinaweza vikanunuliwa toka maduka ya nje ya nchi kwa bei nafuu na vyenye ubora mkubwa.

Kadi za Benki ni nini?

Hizi ni kadi za kuchukulia fedha katika mashine ya kutoa fedha(ATM) ambazo zinakuwezesha pia kununua bidhaa na huduma katika sehemu za mauzo kama mahotelini,maduka ya bidhaa(“Supermarkets”) na katika masoko ya kwenye matandao wa intaneti.
Kadi hizi zimeunganishwa na akaunti yako ya benki na kila unaponunua kupitia kadi hii kiasi cha fedha kinapunguzwa katika akaunti yako sawa na ghramaya bidhaa iliyonunuliwa.
Makampuni ya Benki yanafanya kazi na makampuni ya kimataifa ambayo yanawezesha mfumo huu wa manunuzi kufanya kazi kokote duniani. Baadhi ya makampuni makubwa duniani ni MasterCard na VISA
matumizi-ya-kadi-za-benki_mastercard
Kadi ya MasterCard
matumizi-ya-kadi-za-benki_visa
Kadi ya VISA
 Aina za Kadi:
Kuna aina mbili za kadi za manunuzi
i. Kadi za Malipo ya Mkopo-Creditcard:
Kadi hizi zinaruhusu mteja kununua hata kama hana fedha za kutosha katika akaunti yake na atarudisha mkopo baada ya muda ambao atapangiwa au fedha nyingine inapokuwa imeingia kwenye akaunti hiyo.
Aina hii ya kadi zinatumika zaidi katika nchi zilizoendelea,na aghalabu hutolewa na benki nchini Tanzania.
ii. Kadi za Malipo ya Awali-Debitcard:
Kadi hizi zinamuwezesha mteja kununua kama tu kuna fedha za kutosha katika akaunti yake vinginevyo manunuzi hayatawezekana.
Aina hii ya kadi ndizo ambazo zinatolewa kwa wingi nchini Tanzania.

Matumizi ya kadi za Benki katika Manunuzi:

Nchini Tanzania kwa sasa karibu kadi zote za benki zimeunganishwa na huduma hii na inawawezesha wateja wake wote wenye Kadi za MasterCard au VISA kuweza kununua katika mtandao na katika mashine zilizopo katika maduka na sehemu za huduma mbalimbali kama mahotelini. Pia kadi hizi zinawezesha wateja kutoa fedha katika mashine za fedha (ATM) zozote duniani na kuwawezesha wasafiri kutembea bila fedha wanapokuwa ndani na nje ya nchi.
matumizi-ya-kadi-za-benki_pos-1
Matumizi ya kadi za benki inatoa fursa kwa wafanyabiashara mbalimbali nchini Tanzania na nchi nyingine za Africa kuunganisha machine za malipo ambazo zinaweza kusoma kadi za benki na kurahisisha namna biashara zinanyofanyika.
Huduma za manunuzi ya umeme,mafuta katika vituo vya kuuza mafuta,maduka na hata ulipaji wa kodi mbalimbali. Utumiaji wa mfumo huu katika sehemu za huduma itasaidia kupunguza msongamano wa watu katika sehemu hizi za utoaji huduma kwa jamii.
Pia matumizi ya mfumo huu yatasaidia kupunguza hatari ya kutembea na fedha nyingi na kuvutia wezi barabani na nyumbani.

Faida za Matumizi ya Kadi za Benki Katika Manunuzi

i. Urahisi wa Kupata Huduma
Kutumia kadi kunarahisisha kupata huduma mahala popote, wakati wowote.
Hakuna sababu ya kwenda benki na kusimama katika mstari mrefu.
ii. Unafuu wa Bei
Kwa baadhi ya bidhaa hasa toka nje ya nchi zinaweza kupatikana kwa bei nafuu zaidi kuliko ukinunua toka dukani nchini kwako. Mfano ukinunua kitabu toka Amazon utapata kwa bei nafuu kuliko kununua katika duka la vitabu nchini Tanzania. Hii ni kutokana na gharama za kodi na usambazaji za wauzaji.
 iii. Kupunguza Wizi wa Fedha Taslimu
Ukitumia kadi kwa manunuzi huhitaji kutembea na fedha nyingi mfukoni hivyo kupunguza hatari ya kupoteza au kuibiwa.
iv. Usumbufu wa Kutembea na Fedha Taslimu
Matumizi ya kadi yanaondoa usumbufu wa kutembea na fedha nyingi mfukoni au kutunza majumbani.

 Na Hasara Je?

Kama ilivyo kwa vitu vingine vingi vizuri pia havikosi ubaya kwa upande wa pili:
i. Hatari ya Wizi wa Mtandao
Kumekuwa na matukio ya wizi wa fedha kupitia mtandao na kutumia kadi yako kwa manunuzi kwa jinsi isiyo salama inaongeza hatari ya kuibiwa na wezi katika mtandao.
Hili linaweza kudhubitiwa kwa kuhakikisha unafuata sawa sawa masharti ya usalama kama vile kutogawa namba ya siri kwa yeyote na kutunza kadi sehemu iliyo salama.
 ii. Utegemezi Katika Uwepo wa Mtandao
Kwakuwa kazi zinatumia mtandao kunafanya ukose huduma kama mtandao unakuwa umekatika. Hii inaweza ikakuchelewesha kupata huduma stahiki kwa wakati.
 iii. Kutumia Fedha Kupita Kiasi
Matumizi ya kadi katika manunuzi yanaweza yakakushawishi kutumia zaidi kuliko kama ungetumia fedha taslimu. Hivyo ni muhimu kukuwa na bajeti na kuifuta.
iv. Gharama za Ziada
Kuna gharama za kufanya mwamala katika mtandao ambazo wakati mwingine zinaweza zikafanya bei kuwa kubwa kidogo kuliko kama ungetumia fedha taslimu.

Muda wa Kuhama Umefika?

Bila shaka wakati umefika sasa kwa waafrika kuhamia katika teknolojia hii ya benki,kuna idadi kubwa tayari wanatumia kadi hizi nikiwemo mimi mwenyewe na inaleta mapinduzi makubwa sana kwenye urahisi wa manunuzi na matumizi mazuri ya muda.
Matumizi ya kadi za benki katika mfumo wa manunuzi na malipo itaboresha sekta ya biashara na hata kwa wakulima wa vijijini ambako mtandao wa intaneti umefika au unaweza kufika wataweza kufaidika nayo pia.
Afrika na mataifa yake inapaswa kufahamu kuwa matumizi ya teknolojia kwa njia iliyo sahihi inasaidia sana maendeleo ya nchi kama ambavyo imetokea katika nchi zilizoendelea.
Kama serikali ikitengeneza mfumo mzuri katika taasisi zake kama TRA,Wizara ya fedha,TANESCO na mashirika mengine ya huduma na udhibiti wa fedha ikiwemo benki kuu mfumo huu unaweza ukatumika katika biashara nchini na kuongeza tija na ufanisi.

USHAA IONA HII SASA WAWEZA KUTUMIA SIMU YAKO YA MKONONI KAMA REMORT CONTROL YA TV AU VIFAA VINGINE

KALI%2Bcopy
New Trick
Habari za wakati huu msomaji wa Blog yako pendwa ya DODY BLOG ! Katika mfululizo wa makala za wiki hii, leo tutaangalia jinsi ya KUTUMIA  simu yako hio ya SmartPhonekama Mouse ya kompyuta.

FAIDA
>>>Hii inaweza kukusaidia pale ambapo hauna Mouse kwa ajili ya compyuta yako, au TouchPad ya Laptop yako haifanyi kazi! Yani inasumbua!

MAHITAJI
>>Utahitajika kuinstall program na App ntakazokupa hapa chini! Unaweza kutumia Apps mbalimbali na step ni hizihizi. Host file utaiinstall kwenye kompyuta yako na App utaiweka kwenye simu yako, halafu utaunga compyuta yako kwenye wireless ya simu yako au bluetooth! (Lengo la kuunga ni kuweka mawasiliano kati ya simu na kompyuta). kwa hio unaweza kutumia Bluetooth au Wireless! Zote ni sawa ila hapa nitaelezeaWireless.

HATUA KWA HATUA

1.  Download na install Monect kwenye simu yako HAPA!

2
Install Monect Portable


2. Kwenye PC yako download na install Monect Host kwa kuclik HAPA! File lina MB 28 tuu, kwa hio usiwasingizie Voda. Download na extract vilivyopo kwenye hio Zip File, na chagua lililoandikwaMonectHost, na uliinstall.


3
Download Host


KUMBUKA; Wakati unadownload hio host file, pc yako inaweza kukwambia kwamba hilo file ni Malicious,weka chagua keep file, ili kuweza kuendelea na step za mbele. See picture here>

4
Chagua Keep

>Na pia windows firewall inaweza ikakupa alert, we chagua Allow Access.

5
Allow Access

3. 
Hakikisha simu na kompyuta yako umeviunganisha kwa Wi-fi. Kwenye simu nenda Setting>>>Mobile Networks>>>Tethering and Portable Hotspot, weka settings hapo then iweke ON, na uiunge kwenye PC yako.

4. Tufanye sasa kompyuta na simu yako zipo kwenye Wireless moja, na hio MonectHost umeifungua kwenye kompyuta yako, ifungue ile Monect App ya simu na chagua/click Search Host,ikitokea IP adressya PC yako Connect. Kama unaijua IP ya compyuta yako, unaweza kuiingiza moja kwa moja. Kama inakataa ku connect, jaribu ku restart kompyuta yako na uhakikishe MonectHost umei install vizuri.

6
IP itaonekana ya PC yako

5. Ikishakuwa connected utaona options mbalimbali 12. Kila moja ina kazi yake, leo tutatumia Touch Pad,sababu ndio lengo la makala hii. Tazama picha hapa chini.

7
Options mbalimbali

6. Touch Pad inaifanya simu yako kuwa kama ile Mouse ya Laptop (TouchPad) na inakuwa sehemu ya kutembeza vidole, ku right click, ku scroll ,a ku select kama mouse ya kawaida. Kwa hio ifanyie mazoezi na utakuwa na uwezo wa kuitumia kwa umbali wowote ambapo Wireless itakuwa bado ipo connected.

8


7. Pia kuna options mbalimbali ambazo unaweza pia kuzitumia hapo.

9
Jifunze kuzitumia zote hizi

Kumbuka utaalamu huu umeletwa kwenu kwa ushirikiano wa Technology Homesite na Slaus Technologies Tz1 Team, na kama una swali usisite kutuandikia hapo chini kwenye comments, au wasiliana nasi kwaa njia hizi HAPA!

SOMA MAKALA NYINGINE KAMA HIZI HAPA!