Sunday 22 October 2017

WEKA MATANGAZO YA SEEBAIT KWENYE BLOG YAKO NA ULIPWE

[​IMG]
Habari ndugu zangu katika tech leo tutazungumzia kuhusu kujiinua kiuchumi sisi kama blogger's, nalizungumzia hili baada ya kupata maswali na maoni kuhusu seebait kutoka kwa blogger's wenzangu hivyo tunatimiza Ahadi kama kawaida yetu, naam nisikupotezee wakati twende kwenye mada moja kwa moja.

Jinsi ya kujiunga na seebait hatua kwa hatua hatua ya kwanza ingia kwenye site ya Seebait.com kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Login/SignUp 
[​IMG]
Itaonekana muonekano kama huu pichani
Itakuletea muonekano huo pichani , kwasababu sisi ndio tunahitaji kujipatia pesa kupitia Seebait.com basi tutaenda sehemu iliyoandikwa Select option you want to use kisha chagua mtandao unaohitaji kujisajili seebait kupitia mtandao ulioidhinishwa na seebai ambao ni Facebook, twitter na google+ hivyo nitakuonyesha kupitia google+ kwasababu bloggers wengi tunatumia google+
[​IMG]
ukibonyeza google+ itakuomba idhini hivyo bonyeza Allow, 
[​IMG]
Itakuwezesha kuingia katika dashibodi ya seebait kama inavyoonekana pichani kisha utucopy hizo code na kwenda kuzipaste kwenye blog yako
[​IMG]
Katika dashidadi ya seebait walishakuelekeza sehemu ya kuweka , hivyo ingia kwenye blog yako bonyeza theme kisha edit Html, kisha search maneno haya <head> [ jinsi ya kutafuta code kwenye HTML bonyeza mouse yako mara moja kwenye code za templete yako kisha bonyeza Ctrl+F utaona sehemu ya kusearch] kisha paste code za seebait chini ya code hii <head>. save tempalte yako.
kisha rudi kwenye website ya seebait.com bonyeza sehemu inayosomeka Properties , kisha bonyeza Add Property 
[​IMG]

Utaona fomu kama hiyo hapo juu pichani jaza fomu hiyo kama hapa chini pichani
[​IMG]
Hiyo picha hapo juu ni mfano hivyo jaza kutokana na mahitaji ya blog yako hakikisha hauvunji sheria zaseebait.com, kisha ukimaliza bonyeza Submit
[​IMG]
Ukisha submit itakuletea muonekano huo hapo juu kama umekidhi mahitaji ya seebait , lakini kuna vitu vitapungua kutokana na picha yangu ipo aproved lakini yako haitakuwa aproved kwasababu bado hajakubaliwa na kwenye status itakuonyesha not verify hivyo tumalizie hivi bonyeza sehemu yenye alama ya mshale ulioelekea chini unapatinaka upande wa kulia wa properties yako , utaidownload properties yako kupitia mshale huo, kisha ifungue kwa ku doble-click , itafunguka kupitia browser yako mimi nimetumia Chrome pichani hapa chini
[​IMG]
Utaona code mfano wa hizo hapo juu sasa andaa code zako kwaajili ya ku verify akaunti yako ya seebait , pia seebait wameelekeza kuhusu kukamilisha hilo nenda juu kabisa kulia kwenye dashibodi ya seebait utaona alama ya magazine bonyeza hapo kisha tafuta Property Activation 
[​IMG]
Utaona makala hiyo ya msaada wako imekuwa nambari moja bonyeza neno Read itafunguka makala kisha copy code hii <meta name="seebait" content="ACTIVATION CODE HERE" /> Kisha paste sehemu unayodhani utaweza kuiedit mimi huwa natumia notepad kisha irekebishe hapo kwenye neno ACTIVATION CODE HERE paste zile code za kwenye file ulilodownload kwenye properties hivyo code zako zitakuwa hivi <meta name="seebait" content="ryyady-bhay49d26e96ac7ebfc7c9t.html" /> Chukua code zako hizo ulizozitengeneza vema kisha nenda kapaste chini ya kwenye code hii <head> hii tulishazungumzia sehemu ya kuipata kwenye maelezo yetu hapo juu.

kisha rudi tena kwenye dashibodi ya seebait.com nenda kwenye properties kulia bonyeza alama ya TIKI au Nike utaona mabadiliko sehemu ya status itaandika Active. 
kufikia hapo umefanikiwa kuwa na akaunti ya seebait malizia kuweka matangazo kisha subiri seebait.comwaipitie fomu yako ya maombi kama umekamilisha utakuta notification kwenye dashibodi yako yaseebait.com
[​IMG]
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa sasa jitahidi kutafuta Traffic kwa nguvu ili upate pesa zaidi
All the best

No comments:

Post a Comment