Sunday 22 October 2017

ZIJUE FULSA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Katika makala hii nitazungumzia Biashara ya Mtandao na Fursa Zake. Biashara hii imekuwa ni mojawapo ya aina ya biashara inayowavutia wengi siku za karibuni lakini pia imekuwa ni biashara inayowatisha walio wengi. Makala hii inaelezea  biashara ya mtandao na mbinu za mafanikio.
Related image

Sababu ya wajasiriamali wengi kushindwa katika biashara ni ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya biashara kwa ujumla hususani biashara wanayoifanya. Iwapo wajasiriamali watawekeza muda wao katika elimu ya biashara ya mtandao yamkini wengi watafanikiwa.

Biashara ya Mtandao ni Nini?

Biashara ya Mtandao ni mfumo wa usambazaji wa bidhaa wa kampuni  husika kwenda kwa walaji wake kwa kupitia walaji wanachama kama mawakala.
Mfumo huu unahusisha kusajili watumiaji wa bidhaa kama wanachama katika kampuni na kisha watumiaji hao husambaza habari juu ya bidhaa hizo kwa wengine kuwashawishi wajiunge na kisha kununua bidhaa.
Kampuni husika huwalipa wasambazaji kamisheni kulingana na watu wanaojiunga na kununua bidhaa kupitia kwao.

Fursa Zilizopo katika Biashara ya Mtandao:

Si kazi rahisi kumiliki kampuni au biashara,kuna changamoto nyingi zikiwemo mahitaji ya watu wa kuajiri ili kufanya kazi ,sehemu ya ofisi,sehemu ya kuhifadhi bidhaa kabla hazijasambazwa n.k lakini kupitia makampuni ya mtandao kila mmoja anaweza akaanza biashara kwa mtaji kidogo sana bila kuwa na wasiwasi ya gharama hizo kubwa za kuanzisha biashara binafsi kama katika biashara za kawaida.
Katika biashara ya mtandao unaweza kuanza na mtaji mdogo tu hata chini ya Tsh 500,000/=
Fursa nyingine ni kuwa utapata nafasi ya kukutana na kufanya kazi na watu wenye uzoefu tayari katika biashara ambao wako tayari kukufundisha na kuona kuwa unafanikiwa. Sababu nao wanafanikiwa pale wewe unapofanikiwa.
Katika biashara hii unatumia nguvu kidogo kupata matokeo makubwa kwasababu ya “Nguvu ya Wengi” – Yaani unawatafuta na kuwafundisha wachache ambao nao watafanya hivyo hivyo kwa wengine na hivyo kujenga mtandao mkubwa wa watu chini yako. Lakini ili kujenga timu ya awali utahitaji kufanya kazi kubwa mwanzoni.

Misingi ya Mafanikio Katika Biashara ya Mtandao

Kama ilivyo kwa biashara nyingine yoyote, biashara hii imejengwa kwa misingi hiyo hiyo. Zifuatayo ni misingi mikuu ya kufanikiwa katika biashara ya mtandao:
  1. Wekeza pakubwa ili kupata pakubwa, au wekeza kidogo ili kupata kidogo – Kiasi utakachowekeza katika fedha au muda wako kutatoa matokeo yanayowiana na nguvu zako
  2. Usikate Tamaa Mapema – Ukitaka kufanikiwa ni sharti uvumilie hadi mwisho na usiache, huwezi jua ,pengine pale unapoacha ulikuwa unakaribia mafanikio
  3. Jifunze Elimu ya Biashara – Fahamu namna ya kuwatafuta wateja,kuelezea bidhaa ya kampuni yako na kushawishi wajiunge (Kufunga mauzo). Haya yote utajifunza utakapoanza toka kwa wale wa juu yako,usihofu kama si mzuri bado.
  4. Jenga na Kuza Mtandao wa Watu– Biashara ya Mtandao ni kuhusu mahusiano,unatakiwa kujenga mtandao wa watu ambao wataona na watapenda kufanya unachokifanya.
  5. Uongozi Mzuri – Unatakiwa kuwa kiongozi mzuri unayeenda kwa vitendo. Watu wanapenda kujiunga kwa viongozi wazuri- ni asili yetu.
  6. Fundisha Mbinu za Mafanikio – Wafundishe walio chini yako kufanya kama unavyofanya ili nao wafanikiwe na wewe pia. Utatakiwa kuandaa semina za mafunzo na kuwaalika watu kusikia habari nzuri.

Kuwekeza katika Biashara

Fikiria mbali,kuwa na mawazo ya kijasiriamali na wekeza fedha sehemu ambayo mtaji utakua na kuongezeka. Benki si sehemu sahihi kuweka fedha kwani zinawafaidisha wengine zaidi yako mwenyewe.
Biashara ya mtandao ni sehemu mojawapo ya kuwekeza ili kukuza fedha zako.
Watu wengi wanalalamika kuwa viingilio ni vikubwa (OneCoin: 350,000, Trevo: 466,700) lakini si kweli kwani biashara nyingine za kawaida zinahitaji mtaji mkubwa zaidi. Shida ni pale unapoiangalia Bishara ya Mtandao  “kama si biashara”.
Naomba kuishia hapa kwa leo,bila shaka makala hii itakusaidia kufahamu kuhusu biashara ya mtandao na fursa zake. Tafadhari fanya maamuzi haraka na ujiunge. Hutajutia maamuzi yako.
Pia nitakupa mbinu mbalmbali za kujitangaza kupitia mtandao kama mimi nifanyavyo.
Asante sana na karibu katika Biashara ya Mtandao

Mapendekezo Yangu Juu ya Bisahara ya Mtandao za Kufanya:

Napendekeza kujiunga na kampuni ya Trevo. Pata nafasi usome na kufanya mchanganuo wewe mwenyewe binafsi kulingana na vigezo tajwa katika makala hii.
Tembelea kurasa zifuatazo kujua zaidi kuhusu biashara ya Trevo

No comments:

Post a Comment