Sunday, 22 October 2017

TUMIA INTERNET KWA FAIDA JIFUNZE NJIA ZA KUJIINGIZIA KIPATO KUPITIA MITANDAO

Katika makala hii tutaongelea Nguvu ya Biashara ya Mtandao na Intaneti na namna ambavyo vitu hivi viwili vinapotumiwa kwa pamoja vinavyoweza kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa mtumiaji.
Related image
Bila shaka umeshawahi kusikia kuhusu biashara ya mtandao na intaneti (au wengi tunapenda kuita mtandao). Mara nyingi pia watu wanachanganya kati Biashara ya Mtandao(Network Marketing) na Biashara ya Kwenye Mtandao (Internet Marketing).
Biashara ya Mtandao inahusisha usambazaji wa bidhaa au huduma kwenda kwa watumiaji (walaji) kupitia mdomo toka mtu mmoja ambaye ni mtumiaji au mlaji wa hiyo huduma au bidhaa kwenda kwa mwingine.
Biashara ya Kwenye Mtandao ni biashara ambayo inatumia intanet (mtandao) kama muundo mbinu wa kufanya biashara husika. Mfano wewe unaduka la nguo, na unatumia intanet kutafuta masoko au kuuza. Inaweza ikawa una tovuti ambayo unaonesha bidhaa zako na watu wakiona na kupenda wanakupigia simu ili wakupe oda au wanakuja dukani kununua.
Makala hii inaongelea Biashara ya Mtandao (na sio biashara ya kwenye mtandao) na intaneti. Tunaangalia namna vitu hivi viwili vinavyokupa nguvu kubwa sana ya kutengeneza fedha.

Intaneti ni nini na nguvu zake ni zipi?  

Intaneti ni muunganiko  au mtandao wa komputa au vifaa vya habari na mawasiliano dunia nzima unaowezesha vifaa hivi kutumiana taarifa au kushiriki (share) taarifa hizo.
Intaneti ni muundombinu unaowezesha watu na mashine kuwasiliana kwa urahisi. Imewezesha dunia kuwa kama kijiji kimoja kwa maana ya kuwa muda na umbali sio kikwazo tena kwa watu kuwasiliana. Mtu aliyeko Marekani anaweza akawasiliana na mwingine aliyeko Afrika katika muda mmoja (muda mubashara). Mapinduzi haya yamefanya makampuni na mtu mmoja mmoja kuweza kufanya biashara zao dunia nzima na kupata wateja toka pande zote za dunia na hivyo kukuza uchumi kwa kasi ya ajabu.
Bilionea mmiliki wa Microsoft Bill Gates aliwahisema “Katika karne hii kama biashara yako haiko katika mtandao (intaneti) basi itashindwa”akimaanisha kuwa ili kushindana na kukuza uchumi wa kampuni au biashara yoyote leo ni lazima uhakikishe unatumia nguvu ya intaneti kufanya biashara.
Kwa hiyo ndugu msomaji, kama una biashara au unafikiria kufanya biashara basi hakikisha unaweka mpango mkakati wa kuiweka biashara katika mtandao wa intaneti.
(Wasiliana na Absolute Solutions Ltd – Watengenezaji na Wataalamu wa kupromoti biashara kwenye mtandao wa intaneti)
Nguvu ya Intaneti katika Biashara
Intaneti ina nguvu kubwa satika nyanja tofauti kama mawasiliano ya Radio,TV, barua pepe nk. Ila sisi tutazungumzia katika biashara. Namna amabavyo unaweza kukuza biashara na kipato kutumia intaneti.
Kama nilivyosema hapo awali kwamba kutumia inanet biashara inaweza kuwafikia watu wengi zaidi ukilinganisha na njia nyingine yoyote. Kutumia tovuti,barua pepe au blogu ma mitandao ya kijamii sasa hivi unaweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi sana. Hii ndio nguvu ya intaneti katika kufanya biashara na katika kutafuta fedha.

Biashara ya Mtandao na Nguvu zake Katika Kukuza Kipato

Kama tulivyoona katika utangulizi hapo juu,biashara ya mtandao inahusisha usambazaji wa bidhaa au huduma ili kuwafikia watumiaji toka mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Kwa kiasi kikubwa hii hufanyika kwa njia ya mdomo toka kwa mtu ambaye anatumia bidhaa au huduma kwenda kwa mwingine. Uaminifu na mahusioano mazuri ndio msingi wa biashara ya mtandao.

Nguvu ya Biashara ya Mtandao katika Kipato

Biashara ya mtandao inatoa nafasi kubwa katika kuanza na kukuza biashara yenye kukupa faida katika muda mfupi sana.
Zifuatazo ni baadhi ya faida kubwa za biashara ya mtandao:
  1. Unaweza kuanza na Mtaji Mdogo: Biashara ya mtandao ndio biashara pekee unayoweza kuanza kwa mtaji mdogo sana na yenye uwezo wa kukupa faida kubwa katika muda mfupi. Makampuni mengine unaweza ukaanza hata kwa Tsh 100,000 tu na mengine yana viwango vya juu zaidi.
  2. Uwezo wa kupata Faida Katika Muda Mfupi: Unaweza ukapata faida katika mwezi mmoja tu kulingana na mfumo ambao kampuni inautumia na juhudi unazoweka katika kujenga timu chini yako.  Shida ya wengi katika biashara hii hasa katika nchi za afrika ni kuwa hatuichukulii kama biashara na hivyo kuipa umuhimu mdogo sana. Tunafanya kazi kwa muda mfupi sana, wengine hawaweki hata saa moja katika wiki nzima kitu ambacho kinasababisha kupata matokeo hasi.
  3. Muda Mfupi wa Kazi: Katika biashara hii huhtaji kufanya kazi masaa 8 kama katika ajira. Masaa 2-4 kwa siku yanaweza kukupa matokeo mazuri sana hivyo kutumia muda uliobaki katika siku kufanya mambo mengine ikiwemo kukaa na familia yako au kusafiri.
  4. Kutumia Nguvu ya Watu: Mafanikio katika biashara ya mtandao yanakuja kwa kujenga timu ya watu wanaotumia bidhaa za kampuni husika. Na kufundisha ,na kuhimiza kila mmoja katika timu yako kufanya hivyo hivyo kama unavyofanya wewe. Hii inakufanya usitumie nguvu nyingi sana kupata kipato kama katika kazi nyingine za kujiajiri ambapo mara nyingi inategemea uwepo na nguvu za mtu mmoja.
  5. Uwezo wa Kupata Fedha Nyingi: Biashara hii inauwezo wa kukupa kipato kikubwa katika muda mfupi. Katika muda wa miaka 3-5 uanweza ukapata fedha nyingi sana ambazo huwezi kuzipata katika kazi ya kuajiriwa au hata ajira binafsi na biashara ndogo yoyote. Inakupa uwezo wa kupata hata Tsh Bilioni 1 katika muda wa mwaka mmoja kulingana na kampuni na mfumo unaotumika ka kampuni husika.  [Soma namna ya kutengeneza Tsh Bilioni 1.6 kupitia Biashara ya Mtandao Katika Mwaka 1]
Kwa hiyo kama mtu anataka kukua kiuchumi haraka,biashara ya mtandao ni sehemu muafaka kufikia malengo yake kwa haraka na kuondokana na umasikini.
Lakini ni muhimu kutambua kwamba biashara ya mtandao sio njia ya kuwa tajiri kwa haraka bila ya kufanya kazi. kazi inahitajika hasa katika mwaka wa kwanza unapojenga biashara.

Nguvu ya Biashara ya Mtandao na Intaneti Katika Kukuza Masoko

Tumeona kuwa vyote intaneti na biashara ya mtandao vyote vina nguvu kubwa kwa namna tofauti.
Nguvu ya intaneti ipo katika kusambaza habari kwa haraka na urahisi bila kujali mopaka ya kijiografia na nguvu ya biashara ya mtandao ipo katika kuwezesha kusambaza bidhaa toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa gharama ndogo na kwa ufanisi mkubwa.
Ukijumuisha vitu hivi viwili yaani intaneti na biashara yamtandao utapata matokeo makubwa sana katika mauzo ya bidhaa za kampuni husika.
Unapotumia intanneti kuweza kuwafikia watu wengi juu ya biashara unayofanya unapata wateja wengi au watu wengi watakaoona fursa yako na katika hao wengi pia baadhi yao watajiunga na kununua bidhaa toka katika kampuni yako.
 Hapa intaneti  inamwezesha mwanamtandao kuweza kuwafikia watu wengi wengi ambao anaweza kuanzisha mahusioano nao na hatimaye wakfanya biashara. Mfano mtu anaweza akakutana na mtu mwingine katika mtandao wa kijamii kama facebook au twitter kisha wakajenga mahusiano na baadae wakafanya biashara.
Ukiangalia  hapa hakuna mipaka kwa mtu mmoja ambaye yupo katika biashara ya mtandao katika kuwafikia watu. Hii ndio nguvu ya kufanya boahsra ya mtandao katka intaneti.

Namna za kuwafikia Watu Kupitia Intaneti:

  1. Mitandao ya Kijamii: Matumizi ya facebook,twitter,instagram,pinterest etc  kukutana na kujemga uhusiano nao ambao baadae wanaweza wakawa wateja katika kampuni yako ya mtandao.
  2. Blogu na Tovuti: Tovuti na blogu inawezesha taarifa kuwafikia watu duniani kote. Blogu ni bora zaidi katika kufikisha taarifa nahupendwa sana na watu kutokana na habari zake kubadirika mara kwa mara
  3. Barua Pepe: Ukiwa na anuani nyingi za barua pepe unaweza ukatuma matangazo ya fursa ya biashara yako na kuwafikia watu wengi kwa mara moja. Baadhi yao kati ya hawa watapenda na kujiunga na fursa yako.
  4. Mikutano ya Mbali: Badala ya kukutana na watu ana kwa ana katika mikutano sasa hivi unaweza kufanya mikutano kupitia mtandao wa intaneti hivyo kuondo kiwazo cha wapi mtu au watu walengwa wapo.
Kupitia njia zilizotajwa mwanamtandao anaweza kupata wateja wengi kupitia intaneti.

Kampuni Inayouza Bidhaa Kupitia Mtandao kwa 100% Na namna ya Kujiunga

Makampuni mengi ya biashara ya mtandao yanajitahidi kutumia intaneti, mfano kwa kuelimisha watu na hata kuonesha na kuuza bidhaa zao.
Kampuni ya QNET ni mojawapo ya makampuni machache yanayotumia intaneti kwa 100%. Kampuni hii inaonesha bidhaa na kuziuza mtandaoni hivyo kuwezesha wanachama wake kumilki duka la bidhaa na kuzitangaza duniani kote kupitia tovuti ya kampuni.
Kama unataka kutumia nguvu ya biashara ya mtandao na intaneti basi pata taarifa zaidi kuhusu kampuni hii na ujiunge. Pata taarifa zaidi kuhusu QNET na jinsi ya kujiunga.
[Kwa maswali kuhusu fursa ya QNET wasiliana nami kupitia Whatsapp: 0713 514703 au SMS/Piga 0765 027402 nitakueleza namna ya kufanikiwa katika Biashara ya Mtandao na Intaneti]

Hitimisho:

Mafanikio makubwa katika biashara leo yanaweza kupatikana kama utatumia intaneti. Biashara ya mtandao hali kadharika ni mojawapo ya biashara ambayo kupitia intaneti inakupa nafasi ya kupata watu wengi watakaonunua bidhaa toka katika kampuni yako inayotumia biashara ya mtandao.
Kama wewe upo katika kampuni ya biashara ya mtandao basi anza leo kujenga biashara yako kupitia intaneti ili uweze kufaidika ma nguvu ya intaneti katika kukuza biashara na kipato chako.
Kama umeipenda makala hii juu basi washirikishe na wengine ili wafahamu juu ya Nguvu ya Biashara ya Mtandao na Intaneti kuweza kujipatia kipato. Kama una mawazo ,hoja au maswali basi tuandikie hapa chini.
Biashara njema na tukutane katika makala nyingine.

ZIJUE FULSA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Katika makala hii nitazungumzia Biashara ya Mtandao na Fursa Zake. Biashara hii imekuwa ni mojawapo ya aina ya biashara inayowavutia wengi siku za karibuni lakini pia imekuwa ni biashara inayowatisha walio wengi. Makala hii inaelezea  biashara ya mtandao na mbinu za mafanikio.
Related image

Sababu ya wajasiriamali wengi kushindwa katika biashara ni ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya biashara kwa ujumla hususani biashara wanayoifanya. Iwapo wajasiriamali watawekeza muda wao katika elimu ya biashara ya mtandao yamkini wengi watafanikiwa.

Biashara ya Mtandao ni Nini?

Biashara ya Mtandao ni mfumo wa usambazaji wa bidhaa wa kampuni  husika kwenda kwa walaji wake kwa kupitia walaji wanachama kama mawakala.
Mfumo huu unahusisha kusajili watumiaji wa bidhaa kama wanachama katika kampuni na kisha watumiaji hao husambaza habari juu ya bidhaa hizo kwa wengine kuwashawishi wajiunge na kisha kununua bidhaa.
Kampuni husika huwalipa wasambazaji kamisheni kulingana na watu wanaojiunga na kununua bidhaa kupitia kwao.

Fursa Zilizopo katika Biashara ya Mtandao:

Si kazi rahisi kumiliki kampuni au biashara,kuna changamoto nyingi zikiwemo mahitaji ya watu wa kuajiri ili kufanya kazi ,sehemu ya ofisi,sehemu ya kuhifadhi bidhaa kabla hazijasambazwa n.k lakini kupitia makampuni ya mtandao kila mmoja anaweza akaanza biashara kwa mtaji kidogo sana bila kuwa na wasiwasi ya gharama hizo kubwa za kuanzisha biashara binafsi kama katika biashara za kawaida.
Katika biashara ya mtandao unaweza kuanza na mtaji mdogo tu hata chini ya Tsh 500,000/=
Fursa nyingine ni kuwa utapata nafasi ya kukutana na kufanya kazi na watu wenye uzoefu tayari katika biashara ambao wako tayari kukufundisha na kuona kuwa unafanikiwa. Sababu nao wanafanikiwa pale wewe unapofanikiwa.
Katika biashara hii unatumia nguvu kidogo kupata matokeo makubwa kwasababu ya “Nguvu ya Wengi” – Yaani unawatafuta na kuwafundisha wachache ambao nao watafanya hivyo hivyo kwa wengine na hivyo kujenga mtandao mkubwa wa watu chini yako. Lakini ili kujenga timu ya awali utahitaji kufanya kazi kubwa mwanzoni.

Misingi ya Mafanikio Katika Biashara ya Mtandao

Kama ilivyo kwa biashara nyingine yoyote, biashara hii imejengwa kwa misingi hiyo hiyo. Zifuatayo ni misingi mikuu ya kufanikiwa katika biashara ya mtandao:
  1. Wekeza pakubwa ili kupata pakubwa, au wekeza kidogo ili kupata kidogo – Kiasi utakachowekeza katika fedha au muda wako kutatoa matokeo yanayowiana na nguvu zako
  2. Usikate Tamaa Mapema – Ukitaka kufanikiwa ni sharti uvumilie hadi mwisho na usiache, huwezi jua ,pengine pale unapoacha ulikuwa unakaribia mafanikio
  3. Jifunze Elimu ya Biashara – Fahamu namna ya kuwatafuta wateja,kuelezea bidhaa ya kampuni yako na kushawishi wajiunge (Kufunga mauzo). Haya yote utajifunza utakapoanza toka kwa wale wa juu yako,usihofu kama si mzuri bado.
  4. Jenga na Kuza Mtandao wa Watu– Biashara ya Mtandao ni kuhusu mahusiano,unatakiwa kujenga mtandao wa watu ambao wataona na watapenda kufanya unachokifanya.
  5. Uongozi Mzuri – Unatakiwa kuwa kiongozi mzuri unayeenda kwa vitendo. Watu wanapenda kujiunga kwa viongozi wazuri- ni asili yetu.
  6. Fundisha Mbinu za Mafanikio – Wafundishe walio chini yako kufanya kama unavyofanya ili nao wafanikiwe na wewe pia. Utatakiwa kuandaa semina za mafunzo na kuwaalika watu kusikia habari nzuri.

Kuwekeza katika Biashara

Fikiria mbali,kuwa na mawazo ya kijasiriamali na wekeza fedha sehemu ambayo mtaji utakua na kuongezeka. Benki si sehemu sahihi kuweka fedha kwani zinawafaidisha wengine zaidi yako mwenyewe.
Biashara ya mtandao ni sehemu mojawapo ya kuwekeza ili kukuza fedha zako.
Watu wengi wanalalamika kuwa viingilio ni vikubwa (OneCoin: 350,000, Trevo: 466,700) lakini si kweli kwani biashara nyingine za kawaida zinahitaji mtaji mkubwa zaidi. Shida ni pale unapoiangalia Bishara ya Mtandao  “kama si biashara”.
Naomba kuishia hapa kwa leo,bila shaka makala hii itakusaidia kufahamu kuhusu biashara ya mtandao na fursa zake. Tafadhari fanya maamuzi haraka na ujiunge. Hutajutia maamuzi yako.
Pia nitakupa mbinu mbalmbali za kujitangaza kupitia mtandao kama mimi nifanyavyo.
Asante sana na karibu katika Biashara ya Mtandao

Mapendekezo Yangu Juu ya Bisahara ya Mtandao za Kufanya:

Napendekeza kujiunga na kampuni ya Trevo. Pata nafasi usome na kufanya mchanganuo wewe mwenyewe binafsi kulingana na vigezo tajwa katika makala hii.
Tembelea kurasa zifuatazo kujua zaidi kuhusu biashara ya Trevo

VITU MUHIMU KUWA NAVYO KWENYE SIMU YAKO YA ANDROID



Image result for mobile apps


Matumizi ya simu za SmartPhone yameongezeka sana kote duniani na ikiwemo Tanzania.
Japo simu hizi zinatumika sana ,utafiti unaonyesha kuwa vitu vingi vilivyomo katika simu hizi havitumiwi ipasavyo na baadhi ya watumiaji hata hawajui hata kama simu zao zina uwezo wa kufanya mambo hayo.
SmartPhone ni simu zinazowezesha kuweka au kutoa programu za ziada kuliko zile zilizowekwa na watengenezaji kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali katika simu.
Programu nyingi sana zinatengenezwa kila siku na kuuzwa katika masoko katika mtandao(Android Market na Google Play). Baadhi ya programu hizi ni za bure na zinamuwezesha kila mwenye simu kuweza kuzitumia na kufaidika.
Android ni Programu Mama inayoendesha mfumo wa simu yako aina ya Smartphone. Programu hii imetengenezwa na kumilikiwa na Kampuni ya Google.
Kuna programu za picha,kucheza sauti na video na za kukuwezesha kusoma taarifa mbali mbali.
Hapa tunakuleteeni orodha ya programu za simu ya android 30 ambazo ni muhimu kwa yeyote mwenye simu ya android

Programu 30 Muhimu na Bure za Simu ya Android kwa Yeyote:

1. Merriam Webster

Mojawapo ya kamusi maarufu duniani ya kiingereza kwa kiingereza katika simu yako.
Programu hii inaweza pia kutafuta neno kwa sauti. Inatoa maana ya neno na mifano ya maneno yenye maana sawa(synonyms) na maana tofauti(antonyms). Inatoa mfano wa matumizi na jinsi ya kutamka.

2. MoboPlayer

Inacheza aina nyingi maarufu za video(mp4,mkv,mov na nyingine) na inakuwezesha kutafuta mafaili ya video wakati inapoanzishwa.
Si programu nyingi ambazo zinauwezo wa kufanya hivi,hivyo MoboPlayer ni programu muhimu katika simu yako.
Inauwezo wa kutengeneza orodha ya video katika maktaba yake na hivyo kurahisisha mpangilio na upatikanaji wa mafaili.

3. WebMD

Ni programu inayotoa msaada wa taarifa za kiafya na inakusaidia kufanya maamuzi.
WebMD kwa Android inasaidia kuweza kufahamu juu ya afya yako kwa kukupa taarifa za kiafya ambazo nitakufanya kuchukua hatua sahihi juu ya afya yako.
Ina huduma za kuangalia dalili za magonjwa,ushauri wa dawa na athari zake, msaada juu ya huduma ya kwanza na orodha ya vituo vya huduma ya afya karibu na wewe.

4.Pocket

Katika ulimwengu wa mtandao,utunzaji wa taarifa za siri kama taarifa za benki,barua pepe na tovuti mbalimbali ni changamoto kubwa.
Pocket inakuwezesha kutunza taarifa hizi sehemu moja na kwa usalama. Mtumiaji atatakiwa kukumbuka nenosiri kuu moja tu (master password) kwajili ya kufungua programu ya Pocket.

5. MX Player

Ni programu inayokuwezesha kucheza mafaili ya video na sauti karibu aina zote. Ni rahisi kutumia na inayoaminika.

6. Quickoffice

Inakuwezesha kurekebisha mafaili ya MS excel,word na mengine kwenye simu yako ya android.
Inakuwezesha pia kutuma na kupakua mafaili hayo kwenye hifadhi ya mtandao ya Google Drive ambayo inakuwezesha kupata mafaili yako popote kwenye mtandao wa intaneti.

7. Evernote

Inakuwezesha kuandika maneno,kurekodi sauti,kupiga picha kutumia simu yako na kutunza katika hifadhi ya intaneti na kukuwezesha kusoma mafaili hayo kupitia kompyuta au simu nyingine.
Akaunti ya bure inakuwezesha kuweka hadi kiasi cha MB 60 cha taarifa kwa mwezi. Ukitaka akaunti ya kubwa (proutahitaji kulipia $ 45 kwa mwaka.

8. Last.fm

Last.FM inakuwezesha kusikiliza muziki moja kwa moja toka kwenye intaneti kwenye simu yako.
Pia inakuwezesha kupangilia muziki wako katika orodha unayoipenda.

9. Instagram

Inakuwezesha kupiga picha na video na kuwatumia marafiki kupitia mtandao wa instagram

 10. Flickr

Inakuwezesha kupiga picha na kuwatumia marafiki kupitia mitandao ya jamii kama facebook na twitter.

11. Dropbox

Ni programu inayokuwezesha kutunza taarifa katika hifadhi iliyopo katika mtandao,na kukuwezesha kuzipata kupitia simu au kompyuta tofauti kokote duniani.
Inakuwezesha pia kushiriki na watu wengine ambao utawakaribisha.

 12. Amazon Kindle

Inakuwezesha kusoma vitabu vya kielectroniki katika mtandao toka Amazon-Wauzaji maarufu wa vitabu duniani.

13. Love Film By Post

Kwa wapenzi wa filamu,programu hii inakuwezesha kupangilia taarifa za filamu mbalimbali unazozipenda na kuona vidokezo vyake kupitia simu yako

14. Chrome

Programu inayokuwezesha kuangalia taarifa katika intanet toka Google. Inahitaji Android 4.0 na kuendelea.

 15. TED

Inakuwezesha kuona mazungumzo kwa njia ya video toka katika mtandao maarufu wa www.ted.com
Unaweza kupakua taarifa toka mtandao huu kwenye simu yako bure.

 16. Wikipedia

Inakuwezesha kupata taarifa toka mtandao wa wikipedia.com na kuweza kupakua taarifa katika simu yako na kusoma hata kama hakuna intaneti.

17. FaceBook Messenger

Inakuwezesha kuwasiliana moja kwa moja na marafiki walio kwenye mtandao wa FaceBook bila kuonyesha picha na taarifa nyingine zilizopo kwenye facebook.com.

18. Any.do

Inakuwezesha kupangilia kazi zako za siku na kukukumbusha muda unapofika

 19. VLC for Android Beta

Ni ingizo jipya katika soko. VLC inakuwezesha kucheza video na sauti za aina tofauti katika simu yako.

 20. Comics

Inakupa vichekesho kila siku katika simu.

 21. Viber

Inakuwezesha kutuma ujumbe wa maneno,picha na video kwa watumiaji wengine wa viber bure. Pia inakuwezesha kupiga simu kupitia mtandao wa intaneti bure.

 22. Skype

Inakuwezesha kuwasiliana na watu wengine kupitia mtandao wa intaneti kwa maneno,sauti na video bure.
Pia unaweza kupiga simu yoyote ya mezani na mkononi duniani kote kwa gharama ndogo sana.

23. AppLock

Programu hii inafunga programu nyingine katika simu yako kama sms,majina ya watu katika simu,programu za barua pepe,facebook,programu ya picha na nyinginezo kwa ajili ya kutunza siri zako katika simu.
Usiogope tena kumpa simu rafiki au mtoto, AppLock inakupa uhuru.

 24. Docs To Go 4.0

Inakuwezesha kutunza na kusoma mafaili ya aina tofauti (kama MS Word,PDF n.k) katika simu yako na inakuwezesha kutunza katika hifadhi za mtandaoni.

 25. Mobile Doc Scanner

Ni programu inayokuwezesha kupiga picha taarifa zilizomo katika karatasi au picha na kuziweka katika mfumo wa PDF na kuweza kuzituma kwenye mtandao kupitia barua pepe au hifadhi za mtandaoni.

26. Google Translate

Inakuwezesha kutafsiri maneno toka katika lugha moja kwenda nyingine kutumia simu yako hata bila kuwa na intaneti.
Ina uwezo wa kutafsiri lugha 80

27. Google Goggles

Inauwezo wa kusoma picha na michoro na kutafuta taarifa zake katika mtandao wa google.com
Inauwezo wa kusoma barcode ,QR Code na OCR code na kutafuta taarifa zake katika mtandao.

 28. Google Maps Navigation

Inakuwezesha kuona ramani ya dunia na eneo ulilopo.
Inakuonesha longitudo na latitudo za maeneo mbalimbali likiwemo lile ulilopo. Unaweza kuweka alama katika ramani za sehemu ulizowaji kutembelea.
Pia ina uwezo wa kukupa muelekeo wa njia kama unasafiri au ukiwa umepotea.

 29. Clean Master Phone Boost

Inakusaidia kusafisha simu yako ya Android inapokuwa nzito.
Inaongeza kumbukumbu(RAM na cache) na kuboresha spidi.
Inapunguza joto la simu kwa kusimamisha baadhi ya programu zisizohitajika.

 30. ESPN SportsCenter

Inakupa taarifa mbalimbali za michezo toka kote duniani. Matokeo ya mechi zinazochezwa katika maneno na video.

Orodha ni ndefu na hapa tumetaja chache tu. Je,unaaina nyingine za programu za simu ya android ambazo unatumia na ni nzuri? Tuandikie hapa chini katika sanduku la maoni.
Furahia matumizi ya simu yako. Jaribu programu hizi na ufaidike.

NJIA RAHISI YA KUANZISHA BLOG BURE

Mimi najua, kuanzisha blogu inaweza kuwa na utata. Miaka michache iliyopita, wakati mimi naunda blogu yangu ya kwanza, nilikuwa najua machache kuhusu matumizi ama umuhimu wake. Kwa kuwa nilikuwa ni msomi wa kompyuta hivyo nilishaona mara kwa mara blogu zikitoa maelekezo juu mambo mbalimbali yahusuyo na hata yasiyohusu kompyuta.

Image result for blogger templates
Kwa sasa, nimekuwa nikishuhudia blogu nyingi zikianzishwa, zingine zikiwa na maudhui mazuri na yenye tija kubwa kwa jamii yetu, na nyingine zikiwa hazina cha maana kabisa. Wingi wa blogu na utembelewaji wake unaashiria kiu ya wengi kumiliki blogu na kupashana taarifa mbalimbali.
Ninachoweza kusema ni kwamba kujenga blogu ni rahisi sana na hauhitaji ujuzi wowote kutengeneza tovuti wala kuchapa kodi!.Kwa kweli, mchakato mzima ni kiasi fulani moja kwa moja. Hivyo kama wewe uwe na  umri wa miaka 20 au miaka 70, si jambo – bado unaweza kufanya hivyo ndani ya dakika kumi tu!. Unaweza kufanya hivyo pia, tu kwa kufuata hatua zifuatazo.

TAFADHALI:. Kama utakwama au utahitaji msaada kuanzisha blog yako, usisite kuwasiliana nami, nitakuwa tayari kukusaidia bila shida na kwa gharama nafuu.

Tuanze?

1) AMUA NINI BLOG YAKO ITAHUSU

Jambo la kwanza unahitaji kufanya ni kuchagua mada ya blogu. Je, kuna jambo ungependa watu walifahamu?, Kama ndio, anzisha blogu kuhusu hilo. Ni bora kama wewe umebobea katika nyanja fulani na hata umekuwa kwenye sekta fulani kwa muda mrefu, na kwa sababu hiyo wewe ni mtaalam, unaweza kujaribu blogu itakayoelimisha watu wengine wenye kupenda kuwa kama wewe.
Hata hivyo, kama una wazo lolote ambalo mada yake inaelekeza fursa ya kupata wateja mfano mpishi anaweza kuandika habari za mapishi huku akilenga kupata tenda za mapishi kupitia wasomaji wa blogu yake. Fikiria jambio ulipendalo sana,  au kuwa balozi kuhusu shughuli za kila siku.

2) AMUA NI NAMNA GANI UTAHODHI BLOGU YAKO, UTALIPIA, AU YA BURE?
Awali ya yote, blogu nyingi kwenye mtandao ni kwa kutumia WordPress. Kwa kweli, WordPress imepakuliwa zaidi ya mara milioni 72 na hutumiwa na mabloga wengi maarufu na tovuti mbalimbali ikiwemo na hii unayoisoma sasa.
Ni kwa nini nadhani kutumia WordPress ni njia bora ya kuanza blogu yako:
  • Unaweza kuchagua mandhari (Themes) na mipangilio (Layouts) kutoka kwa watu wengi tofauti na bure.
  • Unaweza kuandika makala kwa urahisi na kuongeza picha / video
  • Una uwezo wa kuandaa kategoria na kujenga orodha makabrasha (Archives)
  • Watu wanaweza kutoa maoni na kushiriki blog yako
  • nk …

  Bure si BURE …

Ndiyo, unaweza kuunda blogu ya bure kwenye blogger.com au tumblr.com , lakini wao si kweli bure. Na napenda kukuambia kwa nini …
Wao wana upungufu wa mandhari nzuri – Kwa maneno mengine, blog yako itakuwa ikionekana tupu na kawaida. Kama unataka mandhari ya ziada au vipachiko (Plugins) vya kuboresha blogu yako, unatakiwa kulipia vitu hivyo.
 Huna udhibiti wa blog yako – blogu yako itakuwa ni mwenyeji kwenye tovuti nyingine, hivyo wewe si “mmiliki” wa mali hii. Kama Wasimamizi wakiamua kwamba blogu yako haiendani na sera zao (ambayo inaweza kutokea mara nyingi kabisa), wanaweza kweli kufuta blogu yako bila maonyo yoyote. Kwa kifupi, kila kazi yako uliyofanya kwa bidii bidii na muda alitumia juu ya blogu itakuwa vimepotea ndani ya sekunde.
Gharama ya kuanzisha BLOGU yenye domain yako mwenyewe NI NINI?
Si sana. Unahitaji domain mfano (jinalako.com) kwa  gharama takriban TShs 30000 kwa mwaka na hosting (huduma unajumuisha blog yako na mtandao) ni karibu TShs 75000 – 150000 kwa mwaka. Jambo zuri kuhusu domain binafsi kwa blogu yako ni kwamba pia utaweza kuwa na mawasiliano ya barua pepe yenye mfano wa jina@lako.com.

3) KUCHAGUA DOMAIN & hosting, na KUANDAA WordPress blog domain yako mwenyewe

Kama aliamua kwenda na blogu yenye  domain yako mwenyewe, utahitaji kuchaguajina la domain yako ambalo litaendana na blogu na pia liwe rahisi kukumbukwa. Kupata jina zuri la domain inaweza kuchukua muda., Lakini ni thamani yake.  Lakini kwa nini?
Watu hawawezi kukumbuka domain muda mrefu na wakati wanataka kurudi kwenye blogu yako kuna uwezekano wa kusahau jina hilo. Ni bora zaidi kuchagua kitu cha kukumbukwa, kama vile www.fashionologie.com, www.vivalafashion.com au kitu sawa. Kama mbadala, unaweza tu kutumia jina lako, kwa mfano:. www.johnkipepeo.com
Kwa kifupi, jina la domain yako lazima:
  • Livutie
  • Rahisi kukumbuka
  • Lakipekee

WAPI NAWEZA KUPATA JINA LA DOMAIN NA HOSTING?

Mimi kawaida hupendekeza watu kupata domain na hosting kutoka sehemu moja, kwa njia ambayo itasaidia kuokoa baadhi ya fedha na wakati. Katika miaka michache iliyopita wakati mimi naanza kujenga na kusimamia blogu mbalimbali, nimegundua kwamba kuna makampuni machache sana yakuaminika.
Kuwa muwazi zaidi, nimekuwa nikitumia makampuni kadhaa katika siku za nyuma. Kutaja baadhi yao: Bluehost, Hostgator, Dreamhost nk LAKINI … Mimi sikuwahi kuridhika na huduma yao. Hivyo kwa urahisi napenda kukuelekeza WEBNERD SOLUTIONS ili upate huduma hizo kwa gharama nafuu.

HITIMSHO
Ni matumaini yangu nimejaribu kukufungulia baadhi ya mambo muhimu yanaweza kukusaidia kama unafikiria kuanzisha blogu yako. Tafadhali kama una swali au maoni tumia fomu iliyo hapo chini kuacha maoni yako au swali lako.