Habari!
Leo niko na habari tofauti kidogo, Tangu ninunue modem kutoka zain nimekuwa nikifurahia huduma zake mno kiasi ya kusema kuwa sina haja ya kununua modem za mitandao mingine, ila kuna kitu sikukiweka akilini mapema. Si muda woote nitakuwa nikiunganishwa, hivyo mara nyingine tena mara kwa mara huwa nakosa huduma ninapoihitaji na wazo hunijia pengine ningekuwa na modem za mitandao tofauti basi ningekuwa na swichi tu.
Kuna njia mbadala kwenye hilo, nikaanza kufuatilia fuatilia kwenye wavuti, nikapata namna ambayo nitaelekeza kupitia ukurasa huu. Na kwa kukumbusha tu ni kwamba, inaweza ikakusaidia au isikusaidie kutokana na kuwa zoezi zima ni la kujaribu kwa nia ya dhati ukiwa tayari kwa matokeo yoyote. Binafsi sikuwa na cha kupoteza wala kusubiri, na kama wengine walijaribu na wakafanikiwa kwa nini mimi niogope au nishindwe. Kama uko na roho/misimamo kama hiyo basi fuata maelekezo haya:-
nenda hapa http://www.bb5.at/huawei.php?imei=<IMEI yako hapa > kama utashindwa kwa njia hiyo hapo, basi inabidi utafute kikokotoo kingine, mimi nilijaribu hiki http://www.mediafire.com/?myfd1zd1cnt kama bado kitashindwa kufanya kazi basi jaribu ku google kwa kutumia model ya modem yako.
Niweke kitu kimoja sawia hapa, kuna modem ambazo zinatumia software inayoitwa MOBILE CONNECT isipokuwa zile za VODACOM kwa hapa kwetu Tanzania. Hizo za mwanzo unachotakiwa ni kuingiza line ya mtandao mwingine tofauti na ulionunulia modem hiyo, Mobile Connect itashindwa kuitambua na hivyo itaomba Unlock code na kutoa majaribio 10 bila shaka, utaingiza namba utakazo zipata kutoka kwenye programu hiyo uliyoishusha ikiwa ulliweka IMEI sahihi ya modem yako.
Kwa wale wengine ambao hawana Mobile Connect watahitajika kutumia http://www.sagmaster.com/download/10SMTi/HUAWEI_MODEM_Code_Writer.rar kupeleka unlock code kwenye modem yako.
Michezo hii yote nmeifanya kwenye modem yangu ya HUWAWEI E1550, kwa wenye model kama hii, nauhakika itakubali tu, tofaui na apo pia nitakuwa nimetoa njia mbadala, unachohitaji ni ku google kwa kutumia jina na model ya modem yako ipasavyo na tangu hapo nimekuwa nikibadilisha line za mitandao tu bila wasiwasi, inanisaidia sana!.
Karibu na Ufurahie tekinolojia
No comments:
Post a Comment