Saturday, 28 September 2019

Apps bora kwa watumiaji wa simu za Iphone

Hivi unajua ni kazi ngumu sana kupekua katika Appstore na kuanza kushusha Apps nyingi nyingi ili upate moja ile ambayo ni nzuri?


Mbali na hapo kama hujawahi kuisikia App ikisifiwa na baadhi ya watu ndio itakua vigumu kabisa kuweza kuelewa kama App hiyo itakua ni nzuri ama la!
Lakini hata hivyo tafiti zimefanyika kwa wale watumiaji wa simu za iOs ni swala ni kwamba, App bora za mwaka 2016 zimefahamika
Fanya Uchunguzi Wa Kina Wa App Kabla Ya Kuishusha
Fanya Uchunguzi Wa Kina Wa App Kabla Ya Kuishusha
Mwingine anaweza akajiuliza ubora wa App uko wapi? Kwa leo sina majibu ya moja kwa moja lakini ningependa tuzione App hizo labda utajifunza kitu
• Evernote
Evernote
Evernote
Hii ni App moja maarufu sana ambayo inamuwezesha mtuamiaji kuweza kuitumia katika kuandika ‘note’ katika kifaa chake. Yaani mtu utakuwa huna haja ya kutembea na peni na daftari au kitu chochote cha kuandika.

Vilevile uzuri wa Evernote ni kwamba hata siku moja huwezi ukapoteza kile unachokiandika miaka na mika kwa sababu unaweza ukakihifadhi katika ile hifadhi ya mtandao (Cloud) na jambo hili ni tofauti kabisa na njia za kawaida tunazotumiaga. Fikiria labda umeandika kitu chako katika daftari lako la kumbukumbu alafu ukalipoteza daftari hilo au labda panya wenye njaa kali wakapita nalo!
• Waze
Waze
Waze
Kwa wale wote ambao wanapenda kusafiri hii sio App ya kuikosa kabisa, hata kwa wale watu ambao kidogo hawaijui mitaa vizuri hii ni App moja ambayo ni nzuri sana kwa ajili yao. Kwa kutumia App hii hata waendesha magari na vyombo vingine vya moto wanaweza wakatonyana mahali ambapo kuna askari wa barabarani. App hii ya Waze ina uwezo wa kujua dereva anaendasha kwa spidi ya kiasi gani na kutoa ushauri kadha wa kadha kuhusiana na barabara.
• 1Password
1Password
1Password
Je wewe ni mmoja kati ya wale ambao kila siku wanasahau password zao? Nawajua watu wengi sana wanaosumbuliwa na hii kitu. Kuna siku simu yangu iliishiwa na chaja nikaomba kwa rafiki yangu iki niingine katika matandao mmoja wa kijamii, ila alichinijibu ni kwamba siwezi fanya hivyo kwani yeye haikumbuki Password yake.
Kwa kutumia 1Password zoezi zima litarahisishwa kwani mtu utakua na kazi ya kuikumbuka password moja tuu na kisha 1Password ndio itachukua jukumu zima la kuzikumbuka password zinigne zote
• IFTTT
If This, Then That (IFTT)
If This, Then That (IFTT)
Wengi wanapata shida na wengine hawajui kabisa ‘if this, then that’ ni kitu gani. Kwa upande wangu sijawahi kutumia App ambayo imetengenezwa kwa akili kama hii. Lakini kumbuka pia tuna mitazamo tofauti tofauti. App hii ukiwa nayo unaweza ukaamuru vitu vingi kufanyika, kwa mfano unaweza ukaamua kuwa kila ukituma picha yako katika mtandao wa kijamii wa Instagram basi picha hiyo ijihifadhi katika hifadhi ya mtandao kama vile Google Drive. Kuna machaguzi mengi unaweza kufanya ukiwa unatumia App hii utaweza kufanya jambo moja na kufanya lingine litokee.
• SwiftKey
SwiftKey
SwiftKey
Hii ni ‘keyboad’ mbadala na kama ukiniuliza mimi basi hii ndio bora kuliko zile zingine zote. Kumbuka kwa kipindi cha muda mrefu sana Apple ilikua hairuhusu utumiaji wa ‘keyboard’ zingine isipokuwa zile ambazo wanatengeneza wao tuu. Hii ilikuja ikabadilika na ndipo hapo Swiftkey walipoingia. Mpaka sasa ndio ‘keyboard’ bora ya mbadala kwa simu za iPhone
• WhatsApp


Hapa sina hata haja ya kuuelezea mtandao huu sana, kwani naamini kila mmoja wetu angalau anautumia mtandao huu kuwasilina na ndugu, jamaa na marafiki. Pia vile vile mtandao huu unajijua kama uko juu ndio maana kila siku unaongeza vipengele mbali mbali ili kuhakikisha kuwa bado unabaki kuwa juu. Hivi karibuni kipengele cha kupiga simu za kuonana kimeongezwa katika mtandoa huo
• Prisma
Prisma
Prisma
Prisma ni moja kati ya App ambazo zimejipatia umaarufu wake katika kipindi cha muda mdogo sana kulinganisha na Apps zingine nyingi ambazo zilisota sana kabla ya kujulikana. Prisma ni App ya kuhariri picha na kuzifanya kuwa na muonekano wa kipekee kabisa
• Snapchat
SnapChat
SnapChat
Snapchat ni mtandao wa kijamii kama vile Instagram tuu lakini mtandao huu uliingia sokoni na kuleta changamoto nyingi sana kwa wapinzani wake kama vile Facebook. Mtandao huu ulipoanza kuliteka soko kwa kiasi flani ndipo hapo mitandao mingine ilipoamua kubadilika na kuongeza vipengele vingine ambavyo pia vilikua vinapatikana katika mtandao huo au la!
• App Za Nyongeza
App ziko nyingi sana ambazo ni nzuri na zimefanya vizuri mwaka 2016 katika simu janja za iPhone, App kama Facebook, Spotify, Adobe Photoshop Fix n.k
Hivi umefikiria kichwani App ambayo unaona imefanya vizuri katika simu za iPhone na haijatajwa hapo juu, kuwa na amani kuitaja hapo chini sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako

No comments:

Post a Comment