CCleaner ni moja ya programu maarufu kwa ajili ya kuwasaidia watumiaji wa kompyuta – kwa Windows na Mac, kusafisha kompyuta zao kwa kuondoa mafaili ya uchafu na yanayojaza nafasi kwenye kompyuta. Ila imefahamika hivi karibuni CCleaner ndiyo ilikuwa ni kirusi pia.
Watafiti wamegundua wadukuzi walifanikiwa kuingia kwenye mtandao wa kampuni inayotengeneza programu hiyo maarufu na kisha kubadilisha faili la programu hiyo kwa kuweka faili ambalo ndani yake wameweka kirusi kwa ajili ya kuathiri kumpyuta za watakaodownload na kutumia programu hiyo.
CClearner ni progrmu (haiuzwi) maalum kwa ajili ya kuondoa cookies kwenye kompyuta na toleo lake la v5.33.6162 lilikuwa na dosari baada ya programu hiyo kudukuliwa na kirusi kuwekwa ndani yake. Takribani wateja mil. 2.2 waliokuwa wamepakuwa toleo la CCleaner v5.33.6162 waliathiriwa na kirusi hicho.
Kompyuta zilizokuwa zimewekwa programu ya CCleaner yenye kirusi ilikuwa ikichukua taarifa za kompyuta husika zilizojumuisha: jina la kompyuta, utambulisho wa kompyuta husika kwenye mtandao (IP address), programu ziliwekwa kwenye kompyua husika, n.k na kuzipeleka taarifa hizo kwenye server iliyopo Marekani.
Kirusi hicho kwenye CCleaner tayari kimeshaondolewa kabla ya kuweza kuleta madhara makubwa kwa watumiaji wa programu hiyo. Imekuwa tabia ya wadukuzi wengi kuanzia mwaka 2016 kudukua programu zenye watumiaji wengi (CCleaner imepakuliwa zaidi ya mara bil. 2).
No comments:
Post a Comment