Dunia nzima inafahamu vuta nikuvute/vikwazo ambavyo Huawei Technologies imekuwa ikikumbana navyo kwa miezi kadhaa kitu ambacho kimechelewesha kuingia sokoni kwa bidhaa mbalimbali hasa zinazotumia 5G.
Tulishaandika mara kadha kuhusu Huawei na simu janja zenye teknolojia ya 5G ingawa zilikuwa bado hazijaingia sokoni mpaka kumi la pili kwa mwezi Julai; Huawei Mate 20X yenye 5G ilitakiwa kuzinduliwa mwezi Juni huko Uingereza lakini kutokana na sababu mbalimbali hilo halikuwezekana. Hata hivyo, inaonekana mambo yameanza kuinyookea kampuni husika kwani simu hiyo imeingia sokoni UK na Umoja wa falme za Kiarabu (UAE).
Je, sifa zake ni zipi?
Huawei Mate 20X (5G) ni simu ambayo bado uzinduzi wake haujafanyika ingawa tayari sifa muhimu zimeshafahamika:
Kipuri mama: Balong 5000 (ndio inayowezesha teknolojia ya 5G kwenye simu husika)
Urefu wa kioo: inchi 7.2 (OLED)
Memori: RAM-GB 8, diski uhifadhi-GB 256
Kamera: Nyuma zipo 3-MP 40, MP 20 na MP 8. Mbele ipo moja-MP 24
Betri: 4200mAh na teknolojia ya kuchaji haraka kiwango cha 40W
Mtandao+Programu endeshi: GSM / HSPA / LTE / 5G. Itakuwa inatumia Android 9
No comments:
Post a Comment