Wednesday 21 October 2020

Chapter 6 DC and AC Machines - ppt video online download

Chapter 6 DC and AC Machines - ppt video online download: Introduction An electrical machine is link between an electrical system and a mechanical system. Conversion from mechanical to electrical: generator Conversion from electrical to mechanical: motor

Chapter 4 Synchronous Generators - ppt video online download

Chapter 4 Synchronous Generators - ppt video online download: Basic Topology In stator, a three-phase winding similar to the one described in chapter 4. Since the main voltage is induced in this winding, it is also called armature winding. In rotor, the magnetic field is generated either by a permanent magnet or by applying dc current to rotor winding. Since rotor is producing the main field, it is also called field winding. Two rotor designs are common: Copyright © The McGraw-Hill Companies, Inc. Permission required for reproduction or display.

Saturday 28 September 2019

Apps bora kwa watumiaji wa simu za Iphone

Hivi unajua ni kazi ngumu sana kupekua katika Appstore na kuanza kushusha Apps nyingi nyingi ili upate moja ile ambayo ni nzuri?


Mbali na hapo kama hujawahi kuisikia App ikisifiwa na baadhi ya watu ndio itakua vigumu kabisa kuweza kuelewa kama App hiyo itakua ni nzuri ama la!
Lakini hata hivyo tafiti zimefanyika kwa wale watumiaji wa simu za iOs ni swala ni kwamba, App bora za mwaka 2016 zimefahamika
Fanya Uchunguzi Wa Kina Wa App Kabla Ya Kuishusha
Fanya Uchunguzi Wa Kina Wa App Kabla Ya Kuishusha
Mwingine anaweza akajiuliza ubora wa App uko wapi? Kwa leo sina majibu ya moja kwa moja lakini ningependa tuzione App hizo labda utajifunza kitu
• Evernote
Evernote
Evernote
Hii ni App moja maarufu sana ambayo inamuwezesha mtuamiaji kuweza kuitumia katika kuandika ‘note’ katika kifaa chake. Yaani mtu utakuwa huna haja ya kutembea na peni na daftari au kitu chochote cha kuandika.

Vilevile uzuri wa Evernote ni kwamba hata siku moja huwezi ukapoteza kile unachokiandika miaka na mika kwa sababu unaweza ukakihifadhi katika ile hifadhi ya mtandao (Cloud) na jambo hili ni tofauti kabisa na njia za kawaida tunazotumiaga. Fikiria labda umeandika kitu chako katika daftari lako la kumbukumbu alafu ukalipoteza daftari hilo au labda panya wenye njaa kali wakapita nalo!
• Waze
Waze
Waze
Kwa wale wote ambao wanapenda kusafiri hii sio App ya kuikosa kabisa, hata kwa wale watu ambao kidogo hawaijui mitaa vizuri hii ni App moja ambayo ni nzuri sana kwa ajili yao. Kwa kutumia App hii hata waendesha magari na vyombo vingine vya moto wanaweza wakatonyana mahali ambapo kuna askari wa barabarani. App hii ya Waze ina uwezo wa kujua dereva anaendasha kwa spidi ya kiasi gani na kutoa ushauri kadha wa kadha kuhusiana na barabara.
• 1Password
1Password
1Password
Je wewe ni mmoja kati ya wale ambao kila siku wanasahau password zao? Nawajua watu wengi sana wanaosumbuliwa na hii kitu. Kuna siku simu yangu iliishiwa na chaja nikaomba kwa rafiki yangu iki niingine katika matandao mmoja wa kijamii, ila alichinijibu ni kwamba siwezi fanya hivyo kwani yeye haikumbuki Password yake.
Kwa kutumia 1Password zoezi zima litarahisishwa kwani mtu utakua na kazi ya kuikumbuka password moja tuu na kisha 1Password ndio itachukua jukumu zima la kuzikumbuka password zinigne zote
• IFTTT
If This, Then That (IFTT)
If This, Then That (IFTT)
Wengi wanapata shida na wengine hawajui kabisa ‘if this, then that’ ni kitu gani. Kwa upande wangu sijawahi kutumia App ambayo imetengenezwa kwa akili kama hii. Lakini kumbuka pia tuna mitazamo tofauti tofauti. App hii ukiwa nayo unaweza ukaamuru vitu vingi kufanyika, kwa mfano unaweza ukaamua kuwa kila ukituma picha yako katika mtandao wa kijamii wa Instagram basi picha hiyo ijihifadhi katika hifadhi ya mtandao kama vile Google Drive. Kuna machaguzi mengi unaweza kufanya ukiwa unatumia App hii utaweza kufanya jambo moja na kufanya lingine litokee.
• SwiftKey
SwiftKey
SwiftKey
Hii ni ‘keyboad’ mbadala na kama ukiniuliza mimi basi hii ndio bora kuliko zile zingine zote. Kumbuka kwa kipindi cha muda mrefu sana Apple ilikua hairuhusu utumiaji wa ‘keyboard’ zingine isipokuwa zile ambazo wanatengeneza wao tuu. Hii ilikuja ikabadilika na ndipo hapo Swiftkey walipoingia. Mpaka sasa ndio ‘keyboard’ bora ya mbadala kwa simu za iPhone
• WhatsApp


Hapa sina hata haja ya kuuelezea mtandao huu sana, kwani naamini kila mmoja wetu angalau anautumia mtandao huu kuwasilina na ndugu, jamaa na marafiki. Pia vile vile mtandao huu unajijua kama uko juu ndio maana kila siku unaongeza vipengele mbali mbali ili kuhakikisha kuwa bado unabaki kuwa juu. Hivi karibuni kipengele cha kupiga simu za kuonana kimeongezwa katika mtandoa huo
• Prisma
Prisma
Prisma
Prisma ni moja kati ya App ambazo zimejipatia umaarufu wake katika kipindi cha muda mdogo sana kulinganisha na Apps zingine nyingi ambazo zilisota sana kabla ya kujulikana. Prisma ni App ya kuhariri picha na kuzifanya kuwa na muonekano wa kipekee kabisa
• Snapchat
SnapChat
SnapChat
Snapchat ni mtandao wa kijamii kama vile Instagram tuu lakini mtandao huu uliingia sokoni na kuleta changamoto nyingi sana kwa wapinzani wake kama vile Facebook. Mtandao huu ulipoanza kuliteka soko kwa kiasi flani ndipo hapo mitandao mingine ilipoamua kubadilika na kuongeza vipengele vingine ambavyo pia vilikua vinapatikana katika mtandao huo au la!
• App Za Nyongeza
App ziko nyingi sana ambazo ni nzuri na zimefanya vizuri mwaka 2016 katika simu janja za iPhone, App kama Facebook, Spotify, Adobe Photoshop Fix n.k
Hivi umefikiria kichwani App ambayo unaona imefanya vizuri katika simu za iPhone na haijatajwa hapo juu, kuwa na amani kuitaja hapo chini sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako

facebook yatambua watumiaji wanaofanya ngono

Je unaweza unaweza kufikiri ni vigumu Facebook kufahamu pale watumiaji wake wanapofanya ngono? Imefahamika si vigumu, na yote yanafanikishwa kupitia mifumo ya data za apps na huduma za matangazo ya Facebook.

Apps za hedhi facebook afya
Katika apps za sekta ya afya ni apps zinazohusisha mizunguko ya hedhi ndio maarufu zaidi
Shirika linalotetea haki za watu dhidi ya teknolojia za kisasa – Privacy International limetoa ripoti inayoonesha tovuti maarufu ya mtandao wa kijamii ya Facebook kwamba huwa unataka kufahamu hadi maisha ya kingono ya watumiaji wake ili kutumia data hizo kwenye huduma zake za kimatangazo.
Apps za uzazi na kufuatilia mizunguko ya hedhi ni maarufu sana hasa hasa kwa wanawake. Ripoti ya Privacy International inaonesha kupitia teknolojia zake za kimatangazo za Facebook zinazowekwa kwenye apps hizo baadhi ya apps maarufu zimekuwa zikituma (kushare) taarifa za watumiaji wake na hali zao hii ikiwa ni pamoja na masuala ya ngono kwenda huduma ya matangazo na data ya Facebook.

facebook na ngono
Facebook na Ngono: Mfano hapa PI waliweza kuona data ambayo mtumiaji aliweka kwenye app ambapo taarifa yake juu ya lengo la kutumia app hiyo ilitumwa kwenda Facebook. Lengo likiwa ‘kupata mimba’
Apps za masuala ya uzazi na kufuatilia mizunguko ya hedhi zimekuwa zikihitaji data/taarifa mbalimbali kutoka kwa mtumiaji ili kuweza kutoa ushauri mzuri zaidi kwa mtumiaji. Baadhi ya data hizo zinahusisha tarehe za mizunguko ya hedhi, na pia kama mwanamke anataka ujauzito basi atakuwa anapata ushauri wa siku za kufanya ngono na yeye kukubali (kutick) au kukataa kama tendo hilo halilifanya – kwa kuweka taarifa hiyo kwenye app hizo.

Apps maarufu zilizokutwa zikifanya hivyo ni pamoja na
    • Maya kutoka kwa Plackal Tech (ina zaidi ya downloads milioni 5 kwenye Google Play),
    • MIA kutoka kwa Mobapp Development Limited (downloads milioni 1) na
    • My Period Tracker iliyotengenezwa na Linchpin Health (downloads zaidi milioni 1 Google Play)
Uchunguzi wa Privacy International umekuta data hizo huwa zinatumwa kwenda kwa baadhi ya makampuni ya kimatangazo na hii ikiwa ni pamoja na Facebook. Iwapo mtumiaji amejiunga kwenye app husika kwa kutumia Facebook (login with Facebook) basi Facebook wanakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kumtumia mtumiaji huyo matangazo pale atakapokuwa anatumia huduma za Facebook au za washirika wa Facebook kupitia kurushiwa matangazo yanayohusiana na maisha yake ya kingono kwa wakati huo.
facebook na ngono
Kwenye app ya Maya ambapo watumiaji huwa pia wanajibu maswali ya ‘Unajisikiaje muda huu’, majibu yao pia yamekuwa yakijumuishwa kwenye data inayotumwa kwenda Facebook
Suala hili ni uvunjifu wa sheria mbalimbali za kimataifa katika mabara ya Ulaya na ata Marekani. Inasemekana muda si mrefu Facebook wanaweza jikuta katika mashtaka kutoka vyombo vya Marekani, Uingereza na Bara la Ulaya (EU).

Suala la ‘Big Data’ – mjumuhisho wa data/taarifa mbalimbali za watumiaji wa intaneti limekuwa changamoto sana kwa sasa. Suala kubwa likiwa ni jinsi gani ya kuhakikisha data za watumiaji wa huduma/mitandao/apps mbalimbali zinakuwa salama na haziendi kutumika nje ya matakwa yao.

Ingawa tayari Ulaya na Marekani wameshaanza kubana huduma mbalimbali za kimtandao kuhakikisha usalama wa data za utumiaji unalindwa bado katika mataifa yaliyoendelea jambo hili haliangaliwi kwa undani zaidi.

Vyanzo: BBC na vyanzo mbalimbali

komputer yako inasumbuliwa na virus CCleaner ndo mkombozi soma zaidi.......

CCleaner ni moja ya programu maarufu kwa ajili ya kuwasaidia watumiaji wa kompyuta – kwa Windows na Mac, kusafisha kompyuta zao kwa kuondoa mafaili ya uchafu na yanayojaza nafasi kwenye kompyuta. Ila imefahamika hivi karibuni CCleaner ndiyo ilikuwa ni kirusi pia.

Watafiti wamegundua wadukuzi walifanikiwa kuingia kwenye mtandao wa kampuni inayotengeneza programu hiyo maarufu na kisha kubadilisha faili la programu hiyo kwa kuweka faili ambalo ndani yake wameweka kirusi kwa ajili ya kuathiri kumpyuta za watakaodownload na kutumia programu hiyo.

CClearner ni progrmu (haiuzwi) maalum kwa ajili ya kuondoa cookies kwenye kompyuta na toleo lake la v5.33.6162 lilikuwa na dosari baada ya programu hiyo kudukuliwa na kirusi kuwekwa ndani yake. Takribani wateja mil. 2.2 waliokuwa wamepakuwa toleo la CCleaner v5.33.6162 waliathiriwa na kirusi hicho.
Kompyuta zilizokuwa zimewekwa programu ya CCleaner yenye kirusi ilikuwa ikichukua taarifa za kompyuta husika zilizojumuisha: jina la kompyuta, utambulisho wa kompyuta husika kwenye mtandao (IP address), programu ziliwekwa kwenye kompyua husika, n.k na kuzipeleka taarifa hizo kwenye server iliyopo Marekani.
CCLeaner
CCLeaner ni programu inayomilikiwa na Avast na ni moja ya programu iliyopakuliwa na watu wengi zaidi. Ipo katika orodha ya programu za kuaminika.
Kirusi hicho kwenye CCleaner tayari kimeshaondolewa kabla ya kuweza kuleta madhara makubwa kwa watumiaji wa programu hiyo. Imekuwa tabia ya wadukuzi wengi kuanzia mwaka 2016 kudukua programu zenye watumiaji wengi (CCleaner imepakuliwa zaidi ya mara bil. 2).

Ni vyema ukaingia gharama ukanunua vitu ambavyo vina dhamana kuliko kupakua programu ya bure kutoka kwenye mtandao; mara nyingi programu hizo huwa ni rahisi kudukuliwa na kuweza kusababisha madhara kwenye kifaa chako.

huawei mate 20x simu janja sokoni

Dunia nzima inafahamu vuta nikuvute/vikwazo ambavyo Huawei Technologies imekuwa ikikumbana navyo kwa miezi kadhaa kitu ambacho kimechelewesha kuingia sokoni kwa bidhaa mbalimbali hasa zinazotumia 5G.

Tulishaandika mara kadha kuhusu Huawei na simu janja zenye teknolojia ya 5G ingawa zilikuwa bado hazijaingia sokoni mpaka kumi la pili kwa mwezi Julai; Huawei Mate 20X yenye 5G ilitakiwa kuzinduliwa mwezi Juni huko Uingereza lakini kutokana na sababu mbalimbali hilo halikuwezekana. Hata hivyo, inaonekana mambo yameanza kuinyookea kampuni husika kwani simu hiyo imeingia sokoni UK na Umoja wa falme za Kiarabu (UAE).


Je, sifa zake ni zipi?

Huawei Mate 20X (5G) ni simu ambayo bado uzinduzi wake haujafanyika ingawa tayari sifa muhimu zimeshafahamika:
Kipuri mamaBalong 5000 (ndio inayowezesha teknolojia ya 5G kwenye simu husika)
Urefu wa kioo: inchi 7.2 (OLED)
Memori: RAM-GB 8, diski uhifadhi-GB 256
Kamera: Nyuma zipo 3-MP 40, MP 20 na MP 8. Mbele ipo moja-MP 24

Betri: 4200mAh na teknolojia ya kuchaji haraka kiwango cha 40W
Mtandao+Programu endeshi: GSM / HSPA / LTE / 5G. Itakuwa inatumia Android 9
Huawei Mate 20X
Huawei Mate 20X (5G) ambayo pia inatumia kalamu janja.

Mpaka sasa rununu (simu janja) husika imeingia sokoni kwenye nchi za Falme za Kiarabu kwa $960|Tsh. 2,246,400. Kiujumla simu husika itazinduliwa Julai 22 2019, Julai 26 itazinduliwa nchini Uchina na itauzwa $1,240|Tsh. 2,901,600.

wamiliki wa magroup ya watsapp kenya kuwa na leseni

Katika kudhibiti majukwaa ya mitandao ya kijamii, watawala nchini kenya wamependekeza muswada ambao utawalazimisha watu walioanzisha makundi ya WhatsApp, Facebook na Wanablogi kuwa na leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano ya Kenya.

Muswada huo ambao tayari umeshapelekwa Bungeni unataka Viongozi (Administrators) wa makundi ya WhatsApp kuwa na leseni na kuwasajili wanachama (Members) wa kundi na pia kujua anuani zao za mahala wanapoishi.

facebook whatsapp apps leseni za whatsapp

Na pia kuweka wazi kile kinachojadiliwa ndani ya kundi kwa jeshi la polisi. Kiongozi wa kundi atalazimika kujaza majina ya wanachama wake pamoja na anuani zao wakati wa kujaza fomu maalumu ya kupata leseni ya uendeshaji wa kundi lake.
Pia Viongozi hao watatakiwa wawe na wanachama waliofikia miaka 18 au zaidi.
Endapo muswada huo utapita basi yeyote atakayeendesha Kundi bila ya Leseni atakumbana na adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja Gerezani au faini ya Kshs 200,000/- (Takribani Tshs 400,000/- )